Kuishi
karne moja au zaidi duniani ni mafanikio makubwa katika maisha ya binadamu.
Lakini
kutokana na kuongezeka sababu zinazopelekea mtu kufa mapema, ikiwemo hali ngumu
ya maisha na kukosa furaha na amani, imeelezwa kuwa ili uishi muda mrefu ni
lazima ufanikiwe katika afya.
Wapo watu waliowahi kuishi
miaka 100 na zaidi na wengine wapo hata sasa, huku wengi wakiwa na siri za
kuishi muda mrefu kiasi hicho.
Mtandao wa indiatime.com kwa
msaada wa watu walioishi kwa miaka mingi duniani, umezitaja siri 7 ambazo
zikizingatiwa zinaweza kumfanya mtu akaishi kwa muda mrefu zaidi.
1: Kutembea sana kwa miguu
George Boggess hakufikisha
miaka 105 lakini aliishi zaidi ya miaka 100 aliwahi kutoa ushauri na siri ya
kuishi umri mrefu kuwa ni kutembea.
2: Kula samaki na kulala kwa
angalau saa 8
Misao Okawa ambaye
alitambulika kama binadamu mwenye umri mkubwa zaidi dunia ambaye alifariki
akiwa na umri wa miaka 117, alisema sushi (samaki) na saa 8 za kulala ni siri
ya kuishi kwa muda mrefu.
3: Kupiga push-ups 5 hadi 7 kila siku
Duranord Veillalord ambaye
alitimiza miaka 109 mwaka jana, anaianza siku yake kwa pushups kila siku.
Pushups,
kikombe cha chai na matunda ni siri ya kuishi kwa miaka mingi.
4: Kaa mbali na vipodozi
Adelina Domingues alikuwa mtu
mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuishi Marekani, ambapo alifariki akiwa na umri
wa miaka 114, anasema siri kubwa ya yeye kuishi miaka mingi ni kujiweka mbali
na vipodozi.
5: Kunywa uji wakati wa kufungua
kinywa
Jesse Gallan aliishi kwa miaka
109 na kusema siri kubwa ilikuwa kunywa uji kama kifungua kinywa chake, pia
alisema kutokuwa na wanaume wengi kwenye maisha yake kuliongeza miaka ya maisha
yake.
6: Kaa mbali na pombe/ulevi
Alexander Imich wa New York
City ambaye aliishi kwa miaka 111, alisema siri kubwa ya yeye kuishi miaka hiyo
ni kwa sababu alijiweka mbali na kilevi na alikuwa muogeleaji na kufanya
mazoezi.
Chakula
chake kilikuwa ni kuku na samaki na kuishi maisha ya kuzingatia kanuni za
kiafya.
7: Kula kwa kiasi
Wanawake wa jamii ya Hunza
inayopatikana katika mipaka ya Kashmir, China na Afghanistan hupata watoto
wakiwa na miaka 60 na wanaume wanaoonekana kama wana miaka 40.
Wazee
wa jamii hii wamefikisha umri wa miaka mia moja na wangali na muonekano kana
kwamba wana miaka 70, ambapo wanajamii hiyo wakisema siri ni kula kwa kiasi.
Wanakula
nyama kidogo katika milo miwili kwa siku.
0 comments:
Post a Comment