Sunday, 5 March 2017

VIDEO: RAIS MAGUFULI ALIVYOAGIZA MKANDARASI ANYANG’ANYWE PASSPORT.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kumnyang’anya Pasi (passport) ya Kusafiria Mkandarasi wa Mradi wa Maji wa Nga’pa hadi atakapomaliza Ujenzi wa mradi huo.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo alipokwenda kukagua mradi huo wa maji ambao hadi sasa umetumia miaka 6 kujengwa lakini bado haujakamilika.
Hata hivyo pamoja na kuchukua pasi hiyo Rais Magufuli amempa miezi minne mkandarasi huyo kuhakikisha mradi unakamilika sambamba na RC Zambi kupewa jukumu la kuhakikisha kuwa mkandarasi hatoki eneo hilo la mradi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment