Saturday, 11 March 2017

MFANYIKAZI WA JELA AFUNGWA KWA KUWA NA UHUSIANO NA MFUNGWA…..

Mwalimu mmoja wa jela ambaye alimpiga busu mbali na kumtumia barua za mapenzi mfungwa aliyeua amefungwa kwa makosa ya ukosefu wa nidhamu katika afisi ya uma.

Sian Doherty mwenye umri wa miaka 24 alikutana na Michael Dobson kupitia kazi yake katika gereza la HMP karibu na soko la Harborough mnamo mwezi Septemba 2015.
Mahakama ya Leicester iliambiwa kwamba Dobson alimtumia ujumbe wa mapenzi huku naye akimwita ''darling'' katika mawasiliano ya simu na akamnunulia simu mpya ili kuficha mawasiliano yao.
Doherty alipewa kifungo cha miezi sita.
Mwalimu huyo wa kuwafunza wafungwa tabia nzuri alipatikana kufuatia wasiwasi kwamba Dobson alikuwa na uhusiano na mfanyikazi mmoja.
Dobson ambaye anahudumia kifungo cha miaka 16 kwa mauaji walitumiana ujumbe na Doherty ikiwemo mmoja uliosema ''unanifanya kujihisi hai mpenzi''.
Kiongozi wa mashtaka Caroline Lody alisema kuwa mfungwa huyo alimwambia Doherty kwamba ''anayachukulia mapenzi yao kwa uzito mkubwa'' huku naye akimjibu ''ni bora kujihisi hivyo''

Katika ujumbe mwengine Dobson alimwambia: ''Siwezi kusubiri kutembelewa nawe ili tupigane busu kwa saa mbili'' huku Doherty akijibu katika ujumbe ambao Bi Lody hakutaka kuusoma mahakamani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment