Wednesday, 15 March 2017

ASILIMIA 34 YA WATOTO HAWANYWI MAZIWA

Asilimia 34 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano wana tatizo la udumavu kutokana na kutokunywa maziwa na kukosa vyakula vyenye virutubisho vya kutosha.

Akizungumza na wadau wa sekta ya maziwa Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Tate Olenasha, alisema hali hiyo inaifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu Afrika kwa kiwango kikubwa cha watoto wenye udumavu, ikitanguliwa na Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
 Alisema uchumi wa taifa hauwezi kuimarika wakati watoto wake wakiwa hawana afya bora inayoweza kuwafanya wakafikiri vizuri na kuwa wabunifu katika shughuli wanazozifanya.
“Kutokana na Watanzania wengi kutokuwa na tabia ya kunywa maziwa, Tanzania kila mwaka inatumia Sh milioni 650 kugharamia matatizo yanayotoka na ukosefu wa lishe bora.
“Udumavu hausababishwi na kukosa chakula tu bali ni kukosekana kwa mlo kamili. Ukinywa maziwa hata glasi  moja unakuwa umepata viinilishe vyote kwa wakati mmoja,” alisema Olenasha.
Alisema wastani wa unywaji maziwa kwa kila Mtanzania kwa mwaka ni lita 47, sawa na mililita 131 kwa siku tofauti na kiwango kilichowekwa na Shirika la Chakula Duniani (FAO) cha lita 200 kwa mwaka.
“Haya yote yanatokea wakati Tanzania ni nchi ya pili Afrika kuwa na mifugo mingi, baada ya Ethiopia. Tuna jiografia nzuri ya malisho, kama tukiweza kuitumia vuziri tutalisaidia taifa kuondokana na udumavu,” alisema Olenasha.
Alisema Serikali inatarajia kuzindua kampeni ya kuhamasisha watu kunywa maziwa yenye kaulimbiu ya ‘Okoa jahazi, jenga afya na uchumi kupitia maziwa’.


Olenasha alisema kampeni hiyo ambayo itakuwa ya nchi nzima, itazinduliwa Mei mwaka huu mkoani Kagera na inatarajiwa kugharimu Sh milioni 380.

Related Posts:

  • MWANAMKE AIKOJOLEA BENDERA YA MAREKANI... Mwanamke aliyesambaza kanda yake ya video akiikojolea bendera ya Marekani ametoa wito kwa watu kutoilenga familia yake akisema hawaungi mkono tendo lake. Emily Lance alipokea vitisho vya mauaji katika mtandao wa kijam… Read More
  • MARUFUKU YA LAPTOP YAONDOLEWA MASHIRIKA 2 YA NDEGE… Mashirika mawili ya ndege ya Kuwait Airways na Royal Jordanian, yameruhusiwa kuruhusu abiria wake kubebea laptop ndani ya ndege zinazoelekea Marekani. Mashirika hayo mawili yamesema yameshirikiana na maafisa wa Mareka… Read More
  • SIMBA 4 WATOROKA MBUGA YA TAIFA.. Walinzi wa mbuga nchini Afrika Kusini wanawattafuta simba wanne waliotoroka kutoka mbuga ya kitaifa. Simba hao walitoroka kutoka mbuga ya Kruger siku ya Jumapili na mara ya mwisho walionekana katika kijiji cha Matsulu. … Read More
  • MELI YA CHINA INAYOBEBA NDEGE ZA KIJESHI IMEWASILI HONG KONG….. Meli ya kwanza ya Uchina ya kubeba ndege za kivita Liaoning imewasili mjini Hong Kong. Ziara hiyo ya kwanza nje ya China bara ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 20 tangu Uingereza ilipoikabidhi Hong Kong kwa China. I… Read More
  • KUTANA NA MWANAMKE ANAYEFUGA NDEVU…. Harnaam Kaur ni mwanamke anayefuga ndevu,na alilianza kufuga ndevu alipokuwa na umri wa miaka 16. “Nilikuwa na nyweIe zilizojaa usoni tangu nibalehe, ikafiki wakati ambapo nilifikiri iwapo nywele hizo zingeendelea kuw… Read More

0 comments:

Post a Comment