Sunday 5 March 2017

NECTA YAZIDI KUWABANA WALIOGHUSHI VYETI

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limeendelea kuwatangazia wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine.

Tangazo hilo limetolewa na NECTA kupitia mtandao wake www.necta.go.tz hatua ambayo inaendeleza juhudi za kuwafichua watumishi ambao wanatumia vyeti ambavyo sio vyao.
Kwa mujibu wa tangazo hilo NECTA imewataka wananchi wenye malalamiko au taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine kuwasiliana nao kupitia barua pepe esnecta@necta.go.tz
Wananchi wametakiwa kufikisha malalamiko au taarifa hizo kwa kuzingatia muda wa saa za kazi kuanzia saa 2:30 Asubuhi hadi 10:30 jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
Aidha, tangazo hilo limesisitiza kuwa kwa msaada zaidi wananchi wawasiliane nao kupitia barua pepe  kwa saa za kazi.
Hata hivyo, tangazo hilo linaendelea kutoa msisitizo kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa Machi 15, 2016 la kuhakiki watumishi wa Umma na kuwaondoa watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo kwa Serikali yake

0 comments:

Post a Comment