Sunday 5 March 2017

TRUMP AMSHUTUMU OBAMA KUMDUKUA…..

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa amegundua Rais mstaafu wa nchi hiyo ambaye ni mtangulizi wake, Barack Obama alikuwa akidukua simu yake mwezi mmoja kabla ya kuchaguliwa
kuliongoza taifa hilo.
Rais Trump ametoa shutuma hizo kupitia ujumbe wake wa Twitter Jumamosi ambapo ameandika kuwa: ‘Makosa sana! Nimegundua kwamba rais Obama alikuwa akidukua simu yangu katika afisi yangu iliopo Trump Tower kabla ya mimi kupata ushindi.’ 
Pamoja na shutuma hizo, Rais Trump hajatoa ushahidi wowote ili kuthibitisha madai hayo ama hata kusema ni agizo gani la mahakama alilonukuu.
Aidha, vyombo vya habari Marekani vimetoa ripoti zinazoeleza kuwa shirika la kijasusi la FBI liliomba agizo la kuwachunguza maafisa wa karibu wa Rais Trump kutoka kwa shirika la kigeni la kijasusi Fisa kubaini iwapo wamekuwa wakiwasiliana na maafisa wa Urusi.
Pamoja na kwamba agizo hilo lilikataliwa lakini baadaye likakubaliwa mwezi Oktoba kulingana na ripoti hizo za vyombo vya habari.

0 comments:

Post a Comment