Sunday, 5 March 2017

NYANYA NDIO TUNDA NI MAARUFU ZAIDI DUNIANI..!

Ikiwa ungeulizwa kutaja tunda bora zaid duniani, labda nyanya haitakuwa akilini mwako.

Lakini unalolihitaji kulifahamu ni kuwa nyanya huzalishwa kwa wingi zaidi duniani kuliko tunda lolote lile.
Baadhi ya watu hudai kuwa tunda la embe ndilo maarufu zaidi duniani kwa misingi kuwa linaliwa kwenye nchi nyingi zaidi kuliko tunda lolote lile.
Lakini ikiwa utapima umaarufu kwa uzalishaji kote duniani, embe liko nyuma ya tufaa nahata ndizi.
Kuna zaidi ya tani 100 za ndizi ambazo huzalishwa kila mwaka huku India ikiwa ndizo mzalishaji mkuu.
Nyanya inaweza kuliwa bia kupikwa au kwa kupikwa. Huku tani 170 za nyanya zikizalishwa kila mwaka, nyanya imeibiku hata ndizi.
Wengi huchukulia nyanya kama mboga lakini ukweli ni kwamba nyaya na tunda kwa sababu ina mbegu hali ambayo huiweka katika familia ya tunda.
Kuna zaidi ya aina 20,000 ya nyanya duniani.
La Tomatina ni sherehe ambazo huandaliwa kila mwaka kwenye mji mdogo wa uhispania wa Bunol.

Wakati wa sherehe hizo karibu watu 40,000 hurushiana nyanya.

0 comments:

Post a Comment