Mahakama nchini Ivory Coast imemwachia huru
first lady wa zamani Simone Gbagbo, aliyekuwa amefungwa kwa makosa dhidi ya
ubinadamu.
Mashtaka yake yalihusiana na vurugu zilizotokea baada ya
uchaguzi wa mwaka 2010, pindi mume wake Laurent alipokataa kushindwa na
Alassane Ouattara.
Majaji wengi wameyapinga mashtaka kuwa Simone Gbagbo 67
aliongoza machafuko hayo, na alijaribu kununua silaha.
First lady huyo alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 20 kwa kuhatarisha
usalama wa nchi.
Ivory Coast imekataa kumpeleka kwenye mahamakama ya kimataifa ya
makosa ya jinai, ambako mume wake Laurent Gbagbo anashtakiwa kwa makosa dhidi
ya ubinadamu.
ICC imetoa agizo la kukamatwa kwa Simone Gbagbo kwa makosa hayo
pia.
Zaidi ya watu elfu 3 walipoteza maisha kwenye vurugu za uchaguzi
nchini humo mwaka 2010.
Laurent na Simone Gbagbo walikamatwa mwaka 2011 baada ya
wanajeshi kuvamia kificho walichokuwemo katika mji mkuu Abidjan.
0 comments:
Post a Comment