Saturday, 11 March 2017

TANZANIA NI NCHI YA MWISHO ULAJI NYAMA A. MASHARIKI…

Pamoja na kwamba Tanzania ni moja ya nchi zenye mifugo mingi barani Afrika, watanzania wanakula nyama kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika ya Mashariki.

Mtanzania anakula kilo 15 kwa mwaka, wakati nchi jirani ya Kenya, mtu anakula kilo 17, Sudan 21 na Bostwana kilo 27.3 kwa mwaka.
Kiwango hicho cha ulaji wa nyama cha Tanzania na nchi hizo nyingine bado ni mdogo ukilinganisha ni kilichowekwa na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) cha ulaji wa wastani wa kilo 50 kwa mwaka kwa mtu.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Maria Mashingo alitoa msisitizo huo mjini hapa wakati akifungua mkutano wa wajumbe wa Baraza la Wadau wa Tasnia ya Nyama nchini.
Maria aliwataka wadau hao kuzisajili kazi zao ili zitambuliwe na watumie mizani ya kisasa (ya kidigitali) na mashine za kukata nyama ili kuwezesha wajali kununua nyama kwenye vipimo vinacholingana.
“Nasisitiza matumizi ya mizani ya kisasa na mashine za kukatia nyama … ili kuwezesha wajali kununua nyama kwa kipimo kinacholinga na uwezo wao kifedha,” alisema.
Aliwataka wafugaji hao wafuge kibiashara kwa kunenepesha mifuko na kuvuna kwa wakati ili kupata mifugo bora kwa ajili ya kuzalisha nyama bora. Maria alizitaka sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa machinjio za kisasa, viwanda vya kusindika nyama na maduka ya nyama yanayokidhi viwango vya ubora.
Alisisitiza kwamba waweke mikakati ya kupunguza kama sio kumaliza kabisa migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na watumiaji wa ardhi wengine, kwa kutambua, kutenga na kuendeleza maeneo malisho na maji ya kutosha. Aliwataka pia watumie mizani na kutumia utaratibu wa kuuza mifugo kwa kunadi ili kuwezesha mifugo kupata bei stahili ya mifugo hiyo.
Tanzania ina wastani wa ng’ombe milioni 25.8, mbuzi milioni 17.1, kondoo milioni 9.2, nguruwe milioni 2.67, kuku wa asili milioni 42.0 na wa kisasa milioni 34.5.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadau wa Tasnia ya Nyama Tanzania, Doreen Maro alisema, mkutano huo unaongozwa na kaulimbiu ya maendeleo endelevu ya viwanda: Fursa za uwekezaji katika mnyororo wa thamani ya nyama.

Doreen aliahidi kwamba atahamasisha ufugaji wa kibiashara na kuvuna kwa wakati ili kupata mifugo bora inayohitajika katika machinjio na viwanda vya kuzalisha nyama bora na kuongeza thamani ya bidhaa hiyo.

Related Posts:

  • BENKI YA FBME YAFUNGWA KWA MADAI YA UTAKATISHAJI WA FEDHA HARAMU…… Benki kuu ya Tanzania inasema kuwa imeipokonya leseni ya kuhudumu benki ya FBME ya Tanzania baada ya kushutumiwa na serikali ya Marekani kwa utakatishaji wa fedha haramu, kulingana na chombo cha habari cha Reuters. Benk… Read More
  • MBARONI AKIPENYEZA SIMU TANO GEREZA LA KEKO DAR… Ramadhani Nombo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Chang’ombe Temeke jijini Dar es Salaam, kwa kosa la kupenyeza simu tano kwenye gereza la Keko. Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya chakula alichopeleka gerezani, … Read More
  • HAJI MANARA ATOA POLE KWA RAIS TFF….. Mara baada ya taarifa kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) kuwashikilia Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa Celestine, kwa tuhuma za… Read More
  • MBARONI KWA KWA UBAKAJI… Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Samweli Masumbuko (32), Mkazi wa Kata ya Mahina wilayani Nyamagana, kwa tuhuma za kumbaka  mwanafunzi wa darasa la pili (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 10. Kwa… Read More
  • DPP ASUBIRI FAILI LA LOWASSA………. Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga, amesema anasubiri Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imalize uchunguzi wake dhidi ya tuhuma zinazomkabili Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Lowa… Read More

0 comments:

Post a Comment