Akiuzungumzia mti huo ambao
unapatikana katika Kijiji cha Tema wilayani Moshi, mtafiti huyo amesema mti huo
ambao ni mrefu kuliko yote barani Afrika una urefu wa mita 81.5 na uko katika
eneo lililopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa).
Dk Andrew amesema kwa mujibu wa utafiti mti huo una uwezo wa
kuishi miaka hiyo kwa kutunzwa na kuhifadhiwa.Amesema kwamba katika utafiti
walioufanya barani Afrika waligundua miti mirefu 31, lakini Mkukusu wa Moshi
ndiyo mrefu kuliko yote na una umri wa miaka 600 hivi sasa ukiwa umevuka
kiwango cha juu cha maisha ya miti ya aina hiyo.
Tayari Serikali imeiagiza Kinapa kuboresha miundombinu ya
barabara ili kuweza kuufikia mti huo iwapo watalii watataka kwenda kuuona.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki amesema mti huo
utasaidia kuongeza mapato kwa kasi kwa kuwa ni kivutio kipya cha utalii ndani
ya mkoa huu.
0 comments:
Post a Comment