Kundi la maseneta wa Italia wametoa wito kwa watengenezaji wa Pizza
nchini humo, kupasi mitihani yao ili kuboresha viwango vya uandaaji wa mlo huo.
Wabunge 22 katika bunge la juu
wamewasilisha mswada bungeni ambao ukipitishwa kuwa sheria, itapendekeza
kusajiliwa kwa taaluma maalum ya pizzaoli (wapishi wa pizza)
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la habari
la Rai,Taaluma hiyo itajumuisha kozi zitakazosomewa kwa jumla ya saa mia moja
ishirini, itakayomuezesha mwanafunzi kufuzu ngazi ya Diploma.
Katika mapendekezo hayo wale
wanaopania kuwa Pizzaoli, wanastahili kupasi mtihani wa nadharia na wa vitendo,
baada ya kusomea sayansi ya chakula,usafi na lugha za kigeni msisitizo zaidi
ukipewa lugha ya kiingereza.
Wale ambao wamekuwa wakitengeza pizza kwa angalau
miaka kumi au zaidi,ambao wanaweza kuungana katika kikundi cha watu wanne moja
kwa moja watatambuliwa kama "master Pizzaoli"
Maseneta hao wanasema karibu
pizza milioni nne huliwa kila siku Nchini Italia, hivyo ipo haja ya kuandaa
pizza inayofikia viwango vya juu.
Italia ina jukumu la kudumisha hadhi yake kwa kuwa
inafahamika kwa uandaaji wa pizza za aina yake duniani.
0 comments:
Post a Comment