Tuesday 23 February 2016

WAFANYAKAZI WATUMBUA JIBU KAMPUNI YA UJENZI ARUSHA…

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Mkulu, ameitakakampuni ya ujenzi ya CATIC kutoka nachini


china, kuhakikisha inawapatia wafanyakazi wake mishahara, mikataba na vitendea kazi kwa mujibu wa sheria ya malipo au mishaara ya mwaka 2013/2014.
Hayo yametokana na mgomo uliofanywa na wafanyakazi hao leo, wakidai kufanya kazi bila mikataba, kupunjwa mishahara, kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
Hali hiyo ilimlazimu mkuu wa wilaya Arusha Fadhili Mkulu, kufika katika eneo ambalo kampuni hiyo inaendelea na ujenzi, na kuzungumza na wahusika wa kampuni hiyo, pamoja na wafanyakazi hao.
Kupitia Kiwale11 Blog,nakupatia fursa ya kuyasikia yale ambayo mkuu wa wilaya ya arusha Fadhili Mkulu, amewataka viongozi wa kampuni hiyo ya ujenzi, kuyatekeleza ndani ya siku saba.
Kwa kubonyeza play hapo chini utasiwasikia wafanyakazi hao wakieleza sababu za mgomo huo, lakini pia utamsikia mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Mkulu.

0 comments:

Post a Comment