Saturday 7 March 2015

WAFANYAKAZI WA RADIO 5 WAPIGWA MSASA NA BBC MEDIA ACTION....

Wafanyakazi wa Radio 5 jijini A rusha wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili
waweze kuandika habari za kuboresha maisha ya jamii kwa kupata maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu,mafunzo hayo yanaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action.

Akizungumza mapema jana katika mafunzo hayo Mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action alisema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kitaaluma pindi wanapokuwa katika kazi zao.

 Alisema kuwa mafunzo hayo yatawezesha pia upatikanaji wa utawala bora kwa kuwa vyombo vya habari vitaelimisha wananchi umuhimu wa kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo Kwa upande wake Msimamizi mkuu wa vipindi vya radio hiyo Mathew Philip alisema kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuwa walikuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo zaidi. 

Pia alisema kuwa kupitia mafunzo hayo wamepata ufahamu wa namna ya kutafuta habari za kupigia kura maoni pamoja na uchaguzi mkuu bila upendeleo kwa kumpa msikilizaji nafasi ya kusikika na kumpa elimu.Mafunzo hayo yalifanyika katika ofisi za radio 5 kwa muda wa wiki mbili.

Wafanyakazi wa kampuni ya Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja jana katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili waweze kuandika habari za kuboresha maisha ya jamii kwa kupata maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu,mafunzo hayo yanaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action, aliyevalia shati la blue ni mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika hilo.

0 comments:

Post a Comment