Tuesday 17 March 2015

Ukatili wa kutisha kichanga chaokotwa kimekufa..!!

Matukio ya kinyama ya kuwatupa watoto hususani vichanga yameendelea kutokea katika maeneo mbali mbali hapa nchini Tanzania.
Jana katika mkoa wa Arusha eneo la  la Relin Themi Njiro, ameokotwa mtoto kichanga ambaye amepatikana akiwa tayari amefariki dunia baada ya kutupwa na mtua ambaye hajafahamika.

Akizungumza na kiwale11blog,diwani wa kata ya Themi venance kinabo,amesema bado haijajulikana mtu aliyemtupa kichanga huyo ametokea eneo gani.

Mtoto huyo amehifadhiwa katika Hospitali ya mkoa wa Arusha Mount meru huku  jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi zaidi


0 comments:

Post a Comment