Thursday, 26 March 2015

Lowassa asema hawezi zuia Mafuriko kwa mikono!!!





Siku moja baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumuonya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa,kwa tuhuma za kukiuka Katiba na kuanza kampeni za Urais kabla ya muda, kiongozi huyo ameibuka na kudai kuwa hana njia ya kuwazuia watu wasimuombe agombee Urais.

Akizungumza na vijana 60 wa bodaboda kutoka wilaya ya Mbarali Mbeya, waliokwenda pia kumshawishi agombee nafasi hiyo mjini Dodoma jana, amesema si vyema kwa maofisa wa chama kuzungumzia masuala ya wanachama wao kwenye vyombo vya habari wakati kuna vikao vya chama.
Awali Kamanda wa Vijana wa CCM wilayani Mbarali Ibrahim Mwakabwanga, ambaye yeye ni kiongozi wa msafara huo kutoka huko, amesema Lowassa hana uwezo wa kushawishi kila kundi na hata wao wamejikusanya wenyewe, wamejigharimia na wameacha shughuli zao na kuamua kuja Dodoma kumshawishi kwa kuwa wanaona ndiye kiongozi ndani ya CCM anayefaa kwa sasa.

Msikie kiongozi wa msafara huo hapo chini
Insert 1-Mwakabwanga

Kwa upande wake lowassa amesema tangu makundi hayo yaanze kujitokeza kumshawishi kuchukua fomu mambo mengi ya ajabu yamesemwa, jambo ambalo linamsikitisha na kumshangaza kwa kuwa endapo kuna mtu wa chama mwenye hoja, ni vyema kuwasilisha kwenye vikao vya chama badala ya kuzungumza hadharani na kwenye vyombo vya habari.

Msikie Mh Lowassa akizungumza hapo chini
Insert 3-Lowassa

Nae bwana Hussein Bashe ambaye mmoja wa wanasiasa vijana hapa nchini,ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa na pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Nzega.
Amezungumzia mengi juu ya haya yanayoenelea kuhusiana na fukuto hili la Urais na kauli kauli mbali mbali zinazoendelea, ambazo amesema ni za kuwatisha watu wengine.

Moja ya kali ambazo amezizungumzia ni zile ambazo zimekuwa zikitolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

Sikia maelezo yake hapo Chini

Insert 5-Bashe




0 comments:

Post a Comment