Watu watano wamefariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, watatu kati yao wakiwamo wanafunzi wawili, wakipoteza maisha baada ya kibanda walichojihifadhi kujikinga na mvua kuangukiwa na nguzo ya umeme na kuwaunguza.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Temeke Zakaria Sebastian, amesema vifo vya watu hao watatu vilitokea katika eneo la Mchikichini Kimbangulile Mbagala.
Amesema wakati mvua ikiendelea kunyesha watu hao walijihifadhi kwenye kibanda kilichotengenezwa kwa mabati, na ghafla waya wa nguzo ya umeme ulikatika na kuangukia kibanda hicho na kushika moto.
Mkugugenzi mtendaji wa Tanecso Mhandisi Felchesmi Mramba,amesema mvua kubwa iliyonyesha imeleta madhara makubwa ikiwemo kusababisha vifo na kutoa tahadhari kwa wananchi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini wasiguse wala kusogelea waya wowote uliodondoka.
Msikie hapa chini anafunguka!!!
0 comments:
Post a Comment