Thursday, 19 March 2015

Mwinjilist akutwa amewahifadhi wahamiaji haramu huko kilimanjaro.....




JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Mwinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Usharika wa Chekereni wilayani Moshi vijiji Mbazi Manase (36) kwa tuhuma za kuwahifadhi wahamiaji haramu wanne raia wa Ethiopia.
Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mwinjilisti hiyo alikuwa amewahifadhi wahamiaji hao katika jiko lake la nyumbani, ikiwa ni sehemu ya hifadhi wakiwa njiani kuelekea Malawi kabla ya kuingia Afrika Kusini kwa lengo la kutafuta maisha mazuri.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela alisema mtuhumiwa huyo na wahamiaji hao wamehifadhiwa katika kituo kidogo cha Polisi cha Himo, nje kidogo ya mji wa Moshi.
Aliwataja wahamiaji hao kuwa ni Atriku Takie (22), Hyelu Agoti (25), Daneze Daiso (30) na Dadaf Eretro (40) wote ni raia wa Ethiopia.
Alisema watuhumiwa wote watano walikamatwa Machi 17 mwaka huu, majira ya saa 7:15 usiku katika kijiji cha Chekereni Tarafa ya Vunjo wilaya ya Moshi Vijijini wakati askari polisi wakifanya doria katika maeneo hayo.

0 comments:

Post a Comment