Monday, 4 April 2016

WAWILI WAFA KWA KUANGUKIWA NA KIFUSI MACHIMBONI….

Watu wawili wameaga dunia baada ya kuangukiwa na kifusi kwenye machimbo haramu ya dhahabu hapo juzi huko katika mkoa wa Geita.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya alasiri juzi Jumamosi, wakati watu watano walipokuwa ndani ya machimbo hayo yanayopatikana katika kijiji cha Busaka katika wilaya ya Chato.
Kamanda Mwabulambo ameongeza kuwa mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya kanda ya ziwa yamedhoofisha kuta za machimbo hayo ya madini na hivyo kusababisha kuporomoka.

Shaaban Ntarambe Mkuu wa wilaya ya Chato ametangaza kufungwa eneo la machimbo hayo. Itafahamika kuwa Geita ni kitovu cha uchimbaji wa madini ya dhahabu nchini Tanzania.

Related Posts:

  • SAMATTA AIBEBA GENK… Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunga bao lake la kwanza Ulaya wakati timu yake Genk ikichapa Club Brugge kwa mabao 3-2 katika Ligi Kuu Ubelgiji. Samatta aliyeingia akitokea benchi katika dakika… Read More
  • IDADI YA WATU YAPUNGUA JAPAN.… Takwimu rasmi ya idadi ya watu nchini Japan, imeashiria kuwa idadi ya watu nchini humo ilipungua kwa takriban watu milioni moja katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Hii ni mara ya kwanza kwa idadi ya watu nchini h… Read More
  • RAIS MPYA WA FIFA NI GIANNI INFANTINO…… Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa. katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wa… Read More
  • MJI WA INDIA WAPIGA MARUFUKU FILAMU…! Mji wa kaskazini mwa India Aligarh, umepiga marufuku filamu mpya yenye jina la mji huo kuoneshwa huko, kwa sababu inahusu mapenzi ya jinsia moja. Meya wa mji huo Shakuntala Bharti amesema jina la filamu linafaa kubadili… Read More
  • UTAFITI: MWANYA KATI YA MATAJIRI NA MASIKINI UNAZIDI KUPANUKA MAREKANI… Utafiti mpya unaonyesha kuwa mwanya kati ya matajiri na masikini unazidi kupanuka nchini Marekani. Gazeti la Wall-Street Journal limechapisha ripoti inayoonyesha kuwa, mlingano wa kijamii unazidi kutokomea miongoni mwa… Read More

0 comments:

Post a Comment