Monday 4 April 2016

ASH SHABAAB YAMNYONGA MTANZANIA…!

Raia wa Tanzania Jemes Mwesiga (27) aliyejiunga na kundi la al Shabaab la nchini Somalia, amenyongwa na kundi hilo kwa tuhuma za ujasusi.


Mtandao wa habari wa Hiiraan Online umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, hukumu ya kifo dhidi ya Issa Jemes Mwesiga (27) aliyejiunga na kundi la Al Shabaab mwaka 2013 ilitekelezwa na kundi hilo siku ya Jumamosi.

Kwa mujibu wa mtandao huo jaji wa mahakama hiyo alisoma hukumu hiyo mbele ya kadamnasi ya watu, kabla ya kutekelezwa adhabu hiyo ya kifo katika uwanja ulio wazi.

Jaji huyo alidai kwenye hukumu yake kwamba mtuhumiwa amekiri makosa kwa kuifanyia ujasusi Marekani, na hivyo amehukumiwa adhabu ya kifo kwa kupigwa risasi.


Mpaka sasa serikali ya Tanzania bado haijasema chochote kuhusiana na habari hiyo.

0 comments:

Post a Comment