Friday 29 April 2016

BALOZI WA SAUDI ARABIA AMEPEWA SAA 48 KUONDOKA ROMANIA…

Balozi wa Saudi Arabia nchini Romania ambaye anakabiliwa na tuhuma ya kumbaka na kumuua
sekretari wake, amepewa masaa 48 afungashe virago na kuondoka nchini humo.

Mtandao mmoja wa Habari nchini humo umeripoti kwamba, Abdulrahman bin Ibrahim alimbaka na kisha kumuua sekretari wake ambaye ni raia wa Romania.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Romania inamtuhumu balozi huyo kuwa, alimbaka Ivan Wilisco binti wa Kiromania mwenye umri wa miaka 25 aliyekuwa akifanya kazi katika ubalozi huo, kama sekretari wa balozi huyo.


Taarifa zaidi zinasema kuwa uchunguzi wa kitiba uliofanywa unaonesha kwamba, binti huyo alibakwa na kisha kunyongwa kwa kutumia mkanda.

0 comments:

Post a Comment