Utafiti mpya umeonesha watu wazima
wengi duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba hakuna matumaini ya kufikia
lengo la kupunguza idadi ya watu wanene duniani.
Wanasayansi
waliofanya utafiti huo ambao walitoka Chuo cha Imperial cha London, wakiandika
katika jarida la kimatibabu la Lancet la Uingereza, wanasema miongo minne
iliyopita, kuwa na uzani wa chini kupita kiasi lilikuwa tatizo kubwa kuliko
unene.
Wanasema
idadi ya wanaume wanene imeongezeka mara tatu, nayo ya wanawake ikaongezeka
mara dufu.
Profesa
Majid Ezzat, aliyeongoza utafiti huo, anasema ni kana kwamba kuna
"mkurupuko wa unene".
Wanasayansi
hao wanaonya kwamba tatizo hilo ni kubwa sana kiasi kwamba haliwezi kutatuliwa
kupitia njia za kawaida za matibabu au kutenga maeneo ya kuendeshea baiskeli.
Wanazihimiza
serikali kuchukua hatua za pamoja, hasa kuhusu bei ya vyakula.
Baada
ya kuchunguza takwimu kutoka nchi 186, watafiti hao walibaini kwamba idadi ya
watu wanene duniani imeongezeka kutoka 105 milioni mwaka 1975 hadi 641 milioni
mwaka 2014.
Idadi
ya watu walio na uzani wa chini ya kuwango imeongezeka kutoka 330 milioni hadi
462 milioni katika kipindi hicho.
Viwango
vya unene miongoni mwa wanaume kilipanda kutoka 3.2% mwaka 1975 hadi 10.8%, na
miongoni mwa wanawake viwango vya unene vilipanda kutoka 6.4 % mwaka 1975 hadi
14.9%.
Hii
ina maana kulikuwa na wanaume wanene 266 milioni na wanawake wanene 375 milioni
mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment