Tuesday 2 June 2015

Simba kapitia dirishani na kuvamia watalii kwenye gari Afrika Kusini… !!!!



 
Vyombo vikubwa vya habari vimeripoti sana hili tukio  leo,kuhusiana na simba aliyepita dirishani na kuvamia watalii kwenye gari huko Afrika Kusini,
kwenye hifadhi ya wanyama ambayo iko kama umbali wa Kilometa 30 hivi toka Johannesburg.
Mtu na mpenzi wake walikuwa ndani ya gari yao wakiwendelea kutalii ndani ya Lion Park, akatokea simba jike mmoja, akawavamia kwenye gari kupitia kwenye dirisha la gari na kumshambulia mwanamke ambaye alifariki kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.
Askari wa hifadhi waliwahi na kuwafukuza simba lakini mwanamke alifariki kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata huku mwanaume akiendelea kupata matibabu.
Tukio la mtu kufariki kutokana na kujeruhiwa na simba hii ni mara ya tatu ndani ya kipindi cha miezi minne ndani ya hifadhi hiyo.

0 comments:

Post a Comment