Thursday 18 June 2015

Sura ya mwanamke kuwa katika noti mpya……

Benki Kuu ya Marekani

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya karne moja, noti mpya ya dola kumi nchini Marekani itakuwa na picha na mwanamke.

Wizara ya Fedha ya Marekani imewataka wananchi wa Marekani,kutoa mawazo yao ni picha ya mwanamke gani ichapishwe kwenye noti hiyo.
Wizara hiyo imesema inatafuta kile kinachoelezwa kuwa demokrasia shirikishi.
Kwa sasa noti za Benki Kuu ya Marekani zilizo katika mzunguko wa fedha, zinawaonyesha viongozi wa zamani wa kisiasa na wote wakiwa ni wazungu.

Noti hiyo mpya ya dola kumi itatolewa nchi humo mwaka 2020, kuadhimisha miaka mia moja ya wanawake wa Marekani kupata haki ya kupiga kura.

0 comments:

Post a Comment