Thursday, 18 June 2015

Roboti kuchukua kazi za raia Australia…!!!

Roboti la muuguzi
Takriban asilimia 40 ya kazi nchini Australia ambazo zipo kwa sasa huenda zikapotea katika kipindi cha kati ya miaka 10 hadi 15 ijayo .

Ripoti mpya ya kamati ya maenedeleo ya kiuchumi CEDA imebaini kwamba matumizi ya mitambo inayojiendesha katika vizazi vijavyo inaweza kubadilisha nguvukazi ya taifa hilo.
Roboti inayotengeza Sandiwichi
Wimbi la mabadiliko ya kiteknolojia halipingiki na linafaa kuchukuliwa kama jeki ya kiuchumi.
Mitambo ya roboti inaweza kuchukua kazi zote kutoka uuguzi hadi upishi,udereva na kuwaosha wagonjwa wazee.

Katika maeneo mengine ya mashambani na majimbo ya Australia zaidi ya asilimia 60 ya kazi zinaweza kupotea kulingana na afisa mkuu wa CEDA Profesa Stephen Martin.

0 comments:

Post a Comment