Friday, 26 June 2015

Mtu mmoja amechinjwa Ufaransa………

Mtu mmoja amechinjwa Ufaransa
Mtu mmoja amechinjwa na mwengine akajeruhiwa vibaya,baada ya shambulizi la kiislamu katika mji wa Lyon Ufaransa.
Vilipuzi kadhaa vilitegwa katika karakana moja iliyoko Saint-Quentin-Fallavier
Mvamizi aliyetekeleza mauaji hayo anasemekana kuwa,alikuwa akipeperusha kibendera cha wanamgambo wa kiislamu.
Kibendera hicho kilipatikana kimetupwa karibu na eneo la tukio.
Mwanaume mmoja amekamatwa na maafisa wa usalama kufuatia tukio hilo.
Wakati huohuo rais wa Ufaransa Francois Hollande, anatarajiwa kukatiza ziara yake rasmi ya viongozi wa bara ulaya na kurejea nyumbani kukabili janga hilo.

Shambulizi hili ni la kwanza tangu lile la kigaidi lililopelekea kuuawa kwa watu 17 miezi sita iliyopita.

Related Posts:

  • SHIRIKA LA NDEGE LAPATA TUZO Shirika la Ndege la Etihad limetajwa kuwa Shirika la Ndege la mwaka, kwenye tuzo nyingine za Business Travel 2016. Tuzo hizo zilitolewa London jana na zilitambua kampuni na watu binafsi, waliopata mafanikio katika sekta… Read More
  • UTAFITI: KUNGUNI HAWASIKII DAWA..! Licha ya kuhusishwa na uchafu na mazingira duni, kunguni ameibuka kuwa mdudu mwenye uwezo mkubwa wa kustahimili hatari dhidi ya maisha yake. Utafiti mpya umebaini kuwa wadudu hao wanaweza kustahimili sio tu tanuri ya mo… Read More
  • MJI WAFURAHIA MTOTO BAADA YA MIAKA 28..! Mji mmoja kaskazini mwa Italia, unasherehekea kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza tangu mapema miaka ya 1980. Meya wa mji wa Ostana ulioko eneo lenye vilima la Piedmont, anasema kuzaliwa kwa mtoto huyo ni kutimia kwa ndoto y… Read More
  • KENYA YASHIKA NAFASI YA 139 KWA UFISADI... Shirika la Transparency International, juzi lilisema kuwa kiwango cha ufisadi kimekuwa kikiongezeka katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Taarifa hiyo ilisema kwamba Rwanda na Tanzania ndiyo mataifa yameibuka k… Read More
  • STORY YA KUOWA WAKE 2 ERITREA NI UZUSHI..!! Habari ya mzaha kwamba wanaume wa taifa la Eritrea wameagizwa kuoa wake wawili, ambayo imesambaa barani Afrika imewaudhi maafisa wa taifa hilo. Afisa mmoja wa ubalozi wa Eritrea Kenya ameiambia BBC kuwa,hata mwendawazim… Read More

0 comments:

Post a Comment