Wanasayansi nchini Uingereza wanasema
kuwa wana ushahidi kwamba watoto wanaodanganya bila mtu kugundua wana
kumbukumbu nzuri ikilinganishwa na wale wasiodanganya.
Watafiti
katika chuo kikuu cha Sheffield kwa siri walichukua filamu ya watoto wa umri wa
miaka sita na saba wakifanya mtihani uliokuwa na majibu ambayo yalikuwa
yameandikwa nyuma ya zao.
Wale
waliodanganya kuhusu kile waliochofanya walifanya vyema kutokana na uwezo wao
kukumbuka walichofunzwa.
Mmoja
ya watafiti hao Elena Hoicka alisema kuwa sababu kuu ni kwamba wale
wanaodanganya hulazimika kukumbuka ukweli wote pamoja na uwongo.
0 comments:
Post a Comment