Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa
Argentine Buenos Aires,kupinga mateso dhidi ya mwanamke.
Maandamano hayo yamefuatia mfulurizo wa visa vya mauaji yaliyoshtua taifa hilo, yakiwemo yale ya mwalimu wa chekechea ambaye bwana yake alimkata koo mbele ya darasa lake.
Vyama vya wafanyakazi, vyama vya kisiasa na kanisa katoliki wameunga mkono maandamano hayo.
Argentina imepitisha sheria dhidi ya unyanyasaji wa nyumbani,lakini wanaharakati wanasema kuwa hazitekelezwi ipasavyo.
Maandamano ya watu wachache pia yamefanyika katika nchi jirani za Chile na Uruguay.
0 comments:
Post a Comment