China ni nchi ambayo adhabu zake kwa wahusika wa dawa za kulevya hazina salia mtume kabisa yaani ukishikwa basi adhabu ya kifo inachukuwa hatamu.
China wana sheria kali sana dhidi ya wahusika wa dawa za
kulevya, ila story nyingine toka huko ni kwamba china sasa ina ongezeko kubwa
la watu wanaitumia dawa za kulevya.
Stori hiyo imeyafungua mengine kwamba kumbe mwaka 2014
idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya iliongezeka ambapo watu elfu 46 na mia 3
waliingia kwenye list ya watu wanaotumia dawa hizo nchini humo.
Ripoti ya China National Narcotics Control Commission ambao wanahusika na udhibiti wa dawa
hizo, inaonesha wengi wao ni vijana ambao umri wao ni chini ya miaka 35.
Kwa sababu China wamejitahidi
sana kuzuia dawa za kulevya kama Cocaine na Heroine kuingia
ndani ya nchi yao, unaambiwa sehemu kubwa watu hao wanatumia dawa ambazo ni
kemikali pamoja na vidonge na watumiaji wenyewe ni watu zaidi ya
Milioni 1.4.
!
0 comments:
Post a Comment