Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah. |
Serikali ya Jamhuri ya
Watu wa China, imeikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
vifaa vya kiufundi vya Sh. bilioni tatu, kwa ajili ya kuiongezea ufanisi zaidi
taasisi hiyo katika vita dhidi ya vitendo vya rushwa.
Vifaa hivyo
vilikabidhiwa na Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing, kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Takukuru Dk. Edward Hoseah, na kushuhudiwa na watendaji wa taasisi hiyo katika
ofisi zake za makao makuu jijini Dar es Salaam jana.
Vifaa hivyo ni
kompyuta za mezani 162 na mpakato 13, printa za mtandao 20, skana 90, UPS
162, servers 4, SAN Storage moja, flashi 10 na simu ya mkononi moja,
vyote vikiwa vya thamani ya Sh. bilioni tatu.
Dk. Hosea aliishukuru
serikali ya China kwa msaada huo akisema vita dhidi ya rushwa inahitaji maamuzi
ya haraka na matumizi ya vifaa vya kisasa ambavyo vina uwezo wa kukabiliana na
wahusika wa vitendo hivyo.
Amesema kutolewa kwa
vifaa hivyo ni uthibitisho dhahiri wa uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili,
na kuahidi kuvitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuongeza
ufanisi katika kukabiliana na baadhi ya changamoto katika utekelezaji wa majukumu
ndani ya taasisi hiyo.
0 comments:
Post a Comment