Rais wa
Shirikisho la Soka Duniani FIFA ametangaza kujiuzulu katika wadhifa
wake huo siku chache tu baada ya kuchaguliwa kwa wingi wa kura kuliongoza
shirikisho hilo.
Hatua
hiyo ya Blatter imewashtua wengi kwani alikuwa amechaguliwa kuongoza
shirika la soka la FIFA kwa muhula wa 5
Ijumaa tarehe 29 mwezi Mei.
Lakini
kuchaguliwa kwake tena kuliongeza shinikizo kutoka kwa mashirika ya soka Ulaya
na baadhi ya wadhamini waliomtaka ajiuzulu kama rais wa FIFA.
Katika
kikao cha waandishi wa habari kilichoandaliwa ghafla hapo jana jioni, Blatter
alitangaza kuwa ataondoka usukani katika miezi michache ijayo na akaitisha
uchaguzi mpya wa kumchagua mrithi wake.
"
Ikumbukwe kuwa punde baada ya kucaghuliwa Ijumaa iliyopita, Blatter alilaani
vikali vyombo vya sheria vya Marekani kwa kuwashtaki maafisa wa shirikisho hilo
kabla ya uchaguzi wa uongozi wake. Aidha aliwakosoa wakuu wa mashirikisho ya
soka ya Ulaya kwa kuendesha kile alichokitaja kuwa ni 'kampeni ya chuki'.
Baadhi
ya wajumbe wa Bunge la Kongresi Marekani wanaishinikiza FIFA ibatilishe uamuzi
wake wa kuipatia Russia haki ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2018.
Blatter
amesema Marekani imeanzisha uchunguzi dhidi ya FIFA baada ya nchi hiyo kunyimwa
haki ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2022.
Hivi
karibuni pia Rais Vladimir Putin wa Russia alikosoa uchunguzi wa Marekani ndani
ya FIFA na kusema, Washington inawashtaki kinyume cha sheria maafisa wa
shirikisho hilo la soka duniani. Amesema huo ni mfano wa wazi wa kiburi na
uingiliaji wa Marekani katika masuala yasiyoihusu.
0 comments:
Post a Comment