Polisi nchini
Argentina wamempiga risasi njiwa ambaye alitumiwa kusafirisha mihadarati kwenda
gereza moja nchini humo, kwa mujibu wa mamlaka za gereza.
Njiwa huyo alionekana akiruka
hadi uwanja wa gereza hilo, lililo katika mji wa Santa Rosa.
Maafisa waligundua kuwa ndege
huyo alikuwa amefungiwa mfuko mdogo kwenye mgongo wake, uliokuwa na vidonge vya
madawa ya kulevya.
Njia hiyo ya kusafirisha
madawa ilikuwa imegunduliwa, na ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi.
Gazeti la
Clarin lilichapisha picha ya njiwa huyo akiwa na mfuko mweupe, uliokuwa na
tembe 44 za madawa ya kulevya.
Magereza nchini Argentina
yalionya mwaka 2013 kuwa, walanguzi wa madawa ya kulevya walikuwa wakitumia
njiwa waliokuwa wakifanya safari mara 10 hadi 15 kwa siku.
Watu watatu walikamatwa na
njiwa 15 kupatikana, baada ya uchunguzi wa mwaka 2013.
Mapema mwaka huu njiwa ambaye
alikuwa na mfuko uliokuwa na tembe 178 za dawa ya kulevya, alishikwa nchini
Kuwait karibu na mpaka na Iraq.
0 comments:
Post a Comment