Mfalme Salman
wa Saudi Arabia ametoa idhini ya wanawake kuendesha magari, hii ikiwa ni kwa
mara ya kwanza katika historia ya taifa. Uamuzi huu umefikiwa kutokana na
harakati za muda mrefu kwa makundi ya wanawake na haki za bindamu kushinikiza
wanawake waruhusiwe kuendesha magari.
Kwa muda mrefu Saudi Arabia
imekuwa nchi pekee Duniani kuwazuia wanawake kuendesha magari. Abdallah
al-Mouallimi Mwakilishi wa umoja wa mataifa kutoka Saudia ametangaza habari
hizi umoja wa huko umoja mataifa.
"Ndugu Mwenyekiti, Mabibi
na mabwana. Najua mtapenda kujua jambo hili kwamba dakika chache zilizopita
Mfalme amepitisha sharia inayowapa idhini,wanawake nchini Saudia kuendesha
magari.Hii ni historia mpya leo kwa jamii ya Saudia,kwa wanaume na wanawake.Na
kwa sasa tunaweza kusema kitu angalau.'' Abdallah al-Mouallimi.
Akizungumza
na waandishi wa msemaji wa idara ya Marekani,Bi.Heather Nauert amelezea kupokea
kwa furaha tangazo hilo.
"Tuna wanafuraha kusikia
jambo hilo,kwamba wanawake wa Saudia sasa wanaruhusiwa kuendesha magari,kwa
hapa Marekani tunafurahia jambo hilo,na kuona ni hatua kubwa na mwelekeo mzuri
kwa taifa hilo'' Heather Nauert.
Mwanaharakati wa Saudi Arabia
aliyewahi wekwa kizuizini kwa siku 73 kutokana na kupinga wanawake kuzuiwa
kuendesha magari, ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter akisema 'Thank you
God', yaani asante Mungu.
Sheria hii inaanza kufanya
kazi mwezi june mwaka ujao, na kwa sasa wizara itatakiwa kuandaa ripoti maalumu
kuhusiana na jambo hilo.
0 comments:
Post a Comment