Ndege
moja aina ya helikopta imeanguka katika ziwa Nakuru nchini Kenya muda mfupi
baada ya kuondoka katika hoteli moja mjini humo.
Afisa mkuu wa Polisi mjini Nakuru
Joshua Omukata amethibitisha kisa hicho akisema kuwa walikuwa wakisubiri boti
kufanya operesheni ya kuwanusuru waliokuwa wakiabiri ndege hiyo.
Ripoti zinasema kuwa kuliwa na
watu watano katika ndege hiyo.
Seneta wa Nakuru Susan Kihika
amesema kuwa watatu kati ya wale waliokuwa wameabiri ndege hiyo walikuwa
wanachama wa kitengo chake cha mawasiliano.
Ndege hiyo iliondoka katika
hoteli ya Jarika County Lodge na duru zinasema kuwa ilikuwa ikipaa chini chini
kabla ya kuanguka.
Ndge hiyo ilitarajiwa kusafrisha
waandishi wa habari katika mkutano wa kampeni .
Waokoaji walikuwa bado hawajaanza
operesheni saa nne baada ya ndege hiyo kuanguka katika ziwa hilo kwa ukosefu wa
boti.
Waokojai walilazimika kusubiri
boti kusafirishwa kutoka Ziwa Naivasha.
Mkurugenzi wa Idara ya kitaifa ya
kukabiliana na majanga Pius Masai amesema kuwa ndege ya polisi imetumwa katika
eneo hilo kusaidia katika uokoaji.
0 comments:
Post a Comment