Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia mganga wa kienyeji
mkazi wa mtaa wa Minga Daud Idd (74), kwa tuhuma ya kunajisi watoto 14 wenye
umri kati ya miaka saba na 12 na kuwasababishia maumivu makali katika sehemu
zao za siri.
Mgonga huyo maarufu kama Babu Karatu ameelezwa kuwa alikuwa
akishirikiana kutenda vitendo hivyo na mtoto wa mdogo wake aitwaye Abdallah
Yahaya (31).
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo
Jumamosi, kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Isaya Mbughi amesema mtuhumiwa
anadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Desemba mwaka jana,
hadi Oktoba mwaka huu.
Amesema kuwa mwathirika mmoja mwenye umri wa miaka saba siku
ya Oktoba 16 mwaka huu saa 11.45 jioni wakati akiogeshwa na mama yake
alilalamika kuwa anasikia maumivu makali katika sehemu yake ya siri.
Amesema baada ya binti kuyo kulalamika kwa mama yake mama
huyo aliweza kumchunguza kwenye sehemu zake za siri na kubaini kuwa michubuko
inayotokana na kuingiliwa kimwili. “Mama huyo baada ya kuona michubuko hiyo
kwenye sehemu za siri za binti yake alimhoji mtoto wake na mtoto huyo aliweza
kumtaja mganga wa kienyeji Karatu.
Mwaathirika huyo alienda mbele zaidi na kumweleza mama yake
kuwa si yeye pekee hufanyiwa vitendo hivyo, bali wapo watoto wengi
wamefanyiwa.”
Kaimu kamanda huyo amesema baada ya hapo mama huyo alitoa
taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa wa Minga na kisha yeye na mwenyekiti wa mtaa
waliweza kuongozana hadi kituo cha kati cha polisi mjini hapa. “Jeshi la polisi
liliweza kuwakamata watuhumiwa hao ambao wanaishi katika nyumba moja, kwa
tuhuma ya ubakaji.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa watoto waliofanyiwa unyama
huo wanasoma katika Shule za Msingi Singidani, Nyerere na Mughanga,”amesema.
Mbughi amesema mbinu iliyokuwa inatumika kuwanasa watoto hao
wa ni kuwarubuni na kisha kuwaonyesha video/movie, kwenye kompyuta mpakato.
0 comments:
Post a Comment