Shirika la
afya duniani WHO limemteuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kama 'balozi mwema '
katika kusaidia kukabiliana na magonjwa yaliyosahaulika.
Akifafanua uamuzi wa uteuzi
huo , Mkurugenzi mkuu mpya wa W.H.O., Dr Tedros Adha-nom Ghebre-yesus, alisifu
namna Zimbabwe inavyozingatia afya ya umma.
Lakini wakosoaji wanasema
katika kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa rais Mugabe, huduma
za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara kwa mara
, na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu.
Dr .Tedros, ni raia wa Ethiopia
ambaye ni Muafrika wa kwanza kuongoza shirika la W.H.O na alichaguliwa kwa
ajili ya kukabiliana na kile kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo
kuwa la kisiasa.
0 comments:
Post a Comment