Mkuu wa
mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli
kuhakikisha anasimamia ujenzi wa Ofisi za Kata na unakamilika kabla ya mwezi wa
kumi na mbili mwaka huu.
Agizo hilo
amelitoa kwenye ziara yake ya siku mbili wilayani Monduli baada ya kujionea
juhudi za wananchi wa Kata ya Moita kwa kufanikisha ujenzi wa Ofisi ya Kata kwa
nguvu zao wenyewe.
Mkuu huyo wa Mkoa aliahidi
kumkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo shilingi milioni kumi kwaajili ya
kumalizia ujenzi huo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za wananchi ambao
wanajitolea kwaajili ya kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Aidha Gambo pia amefanikisha
ujenzi wa darasa moja katika shule ya msingi Kilimatinde baada ya kuchangia
mabati 60, wakati Wananchi wengine wawili wakatoa milioni 4 kwaajili ya tofali
pamoja na mifuko 30 ya Theluji iliyotolewa na Chama cha Mapinduzi wilayani
humo.
0 comments:
Post a Comment