Dubai
imefanya jaribio la teksi ya kwanza ya ndege isio na rubani ambayo wanatumaini
itatumika kama chombo cha uchukuzi mijini.
Ndege hiyo isio na rubani yenye
nafasi ya watu wawili iliruka kwa dakika tano katika pwani ya ghuba.
Ndege hiyo ilitazamwa ikipaa angani
na mwanamfalme Hamdan bin Mohammed.
Dubai ina malengo makubwa ya kuwa
mji wa kiteknolojia huku ndege zisizo na rubani na roboti zikihusika pakubwa
katika mpango huo.
Ndege hiyo ya teksi ilibuniwa na
kampuni ya Ujerumani ya Volocopter na kampuni hiyo imesema inatumai kwamba
ndege hiyo itaanza kufanya kazi katika kipindi cha miaka mitano.
''Utumizi wake utahusisha simu aina
ya smartophone, programu na kuagiza ndege hiyo kuruka hadi katika eneo
unalopania kuelekea'', alisema Afisa mtendaji wa kampuni hiyo Florian Reuter.
Teksi ndege
isiokuwa na rubani awali ilifanyiwa majaribio nchini Ujerumani mnamo mwezi
Aprili.
Kampuni pinzani ya China eHand
ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuzindua msafara wa teksi ndege mjini humo lakini
mipango yake ikaonekana kuchelewa.
Dubai imejiweka kuwa mji wa
kiteknolojia duniani ikiwa na mipango ya magari ya kujiendesha kusimamia robo
ya safari zote kufikia 2030.
Noel Sharkey ambaye ni
mwanasayansi wa komyuta na ambaye pia ni mtaalam wa roboti katika chuo kikuu
cha Sheffield alisema kuwa: Changamoo kuu itakuwa vikwazo visivyoepukika kama
vile kukwepa teksi nyengine, majumba marefu, vindege na ndege zisizokuwa na
rubani ambazo zinatumika kusafirisha mizigo.
0 comments:
Post a Comment