Watu wanne wameuawa kwa kukatwa
vichwa vyao katika eneo la Hindi kaunti ya Lamu, Kenya usiku wa kuamkia
Jumatano.
Kulingana na wanakijiji watu waliokuwa wamevalia magwanda
ya polisi walivamia vijiji viwili vya Bobo na Silini ambako inadaiwa waliwaita
kwa majina watu hao kabla ya kuwatendea nyama huo.
Kamanda wa polisi kaunti ya Lamu
Gilbert Kitiyo amethibitisha tukio hilo huku akisema kuwa wanaendelea na
uchunguzi kubainisha ikiwa mauaji hayo yalitekelezwa na Al Shabaab au wahalifu
katika eneo hilo.
Duru zinadokeza kuwa huenda
mauaji hayo yametokana na mzozo kati ya jamii ya wafugaji na wakulima ambao
huzozania sehemu za kuendeleza shughuli zao.
Wakaazi katika maeneo ya Hindi na Lamu wamefanya
maandamano wakilalamikia utepetevu wa maafisa wa polisi ambao walikosa kufika
kwa haraka hata baada ya wanakijiji kupiga kamsa.
Usafiri wa mabasi kutoka eneo la Mpeketoni Lamu kuelekea
Mombasa imetatizika kwa ajili ya maandamano huku hali ya usalama katika
barabara hiyo ikiwa bado ni hatari kutokana na vilipuzi vya kuwekwa ardhini.
Hali hiyo imetatiza
usafiri wa mabasi na hata magari ya kibinafsi ambapo maafisa wa kijeshi ni
lazima kuyasindikiza magari hayo.
0 comments:
Post a Comment