Saturday 26 May 2018

MHUDUMU WA HOTELI AKUTWA NA SARE ZA POLISI, BASTOLA..!

Mhudumu wa Hoteli ya Sleep Inn na mkazi wa Mwananyamala kwa kopa, anashikiliwa na polisi  kwa kukutwa na sare za  polisi, silaha, cheo cha koplo na pingu.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, imesema Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna mtu mmoja  anatumia sare za Jeshi la Polisi kuwakamata watu na kuwafunga pingu, kuwatishia bastola ili kufanikisha  kupora mali maeneo mbalimbali ya Jiji.
Mambosasa amesema baada ya kufanya naye mahojiano mtumiwa alikiri kumiliki sare na vifaa mbalimbali vya Jeshi la Polisi, na kukubali kuwapeleka askari hadi nyumba anayoishi.
Baada ya kufanya upekuzi kwenye nyumba hiyo alikutwa na sare za Jeshi la Polisi, pingu, cheo cha koplo wa Polisi, mfuko wa kuhifadhia bastola na bastola aina ya GLOCK 17 ambayo imefutwa namba zake za usajili ikiwa haina risasi.
Mtuhumiwa huyo ameshafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

0 comments:

Post a Comment