Monday 3 April 2017

UTAFITI: MANYANYASO HUSABABISHA MTOTO KUPEVUKA MAPEMA

Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Penn State Marekani, wamegundua jambo ambalo linawashangaza wengi katika swala la malezi kwa watoto.


Katika utafiti wao wamesema kuwa zaidi ya 90% ya watoto waliopitia maisha ya kunyanyaswa, kupigwa au kudhalilishwa kingono, wanapevuka haraka ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo.

Professor Jennie Noll aliliambia Jarida la Adolescent Health kuwa, watoto hasa wa kike hupevuka kabla ya muda, pia watoto wa aina hii huota matiti mapema ukilinganisha na watoto wa kawaida.

Akielezea uhusiano ulipo baina ya mtoto kunyanyaswa na kupevuka kabla ya wakati, Dr Noll amesema watoto wanaokuwa katika mazingira kama hayo huzalisha homoni nyingi zinazotokana na msongo mkubwa wa mawazo, hivyo kuharakisha muda wa kupevuka.

Wanasaikolojia hao pia wamesema mtoto anayenyanyaswa yuko hatarini zaidi kupata saratani ya ovary na matiti, ukilinganisha na watoto ambao hulelewa kwenye mazingira ya upendo na amani.

0 comments:

Post a Comment