Saturday 1 April 2017

UTAFITI: UKIOGA KWA MAJI YA MOTO NI MAZOEZI TOSHA....

Watu wengi hupendelea kuoga kwa maji ya moto ili kuepusha maradhi ya kifua wakati wa msimu wa
baridi kali lakini pia kuna faida nyingine ya kiafya inayopatikana ukioga kwa kutumia maji hayo  hivi karibuni Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Loughborough wamegundua kuoga kwa maji ya moto ni sawa na kufanya mazoezi kwa saa moja.
Kwa mujibu wa utafiti huo faida za kiafya kama kupunguza kiasi cha sukari mwilini husaidia mwili kutengeneza homoni inayojulikana kama Metabolism inayosaidia mwili kupungua.
Ili kukamilisha utafiti huu watu 40 walitumika kuoga kwenye maji ya moto yenye nyuzi joto 40 na wote walionekana kupunguza mafuta (Calories) 140 ambayo ni sawa na kukimbia kwa saa moja.
Utafiti huu pia umesema kuwa kuoga kwa maji ya moto kunasaidia kuimarisha mfumo wa upumuaji, kukuepusha na shinikizo la damu na ugonjwa wa kisukari

0 comments:

Post a Comment