Sunday, 9 April 2017

UNYEVU UMEGUNDULIWA NA WANASAYANSI KATIKA SAYARI ILIO SAWA NA DUNIA..

Wanasayansi wanasema kwa mara ya kwanza wamegundua kuna unyevu unaoizunguka sayari ilio kama dunia.

Wameichunguza sayari hii inayotambulika kama GJ 1132b ambayo ukubwa wake ni zaidi ya dunia kwa mara 1.4 na iko umbali wa miaka 39 ya kasi ya muanga.
Uchunguzi wao unaonyesha kuwa sayari hii imezingirwa na gesi ya methane au maji au mchanganyiko wa zote mbili.
Habari hii ni muhimu sana kwa kuendeleza masomo yanayohusiana na maisha nje ya mfumo wa jua. Hata hivyo kuna uwezekano kuwa mtu hawezi kuishi katika dunia hii kwa sababu ya joto jingi la 370C.
Dkt. John Southworth ni mtafiti mkuu kutoka chuo kikuu cha Keele na anasema: "Kulingana na maarifa niliyo nayo, joto la juu zaidi ambalo mwanadamu ameweza kustahimili hapa duniani ni 120C."
Kugunduliwa kwa sayari ya GJ 1132b kulitangazwa kwanza mwaka wa 2015. Sayari hii iko katika mkusanyiko wa Vela, anga ya kusini.
Ingawa ukubwa wake ni sawa na dunia, nyota inayozunguka ni ndogo na yenye mwanga mdogo kuliko jua.
Wakitumia darubini huko Chile, watafiti hao waliweza kuisoma sayari kwa kutazama jinsi ilizuia mwanga wa nyota nyingine zilizopita mbele yake.
Watafiti wanasema kuwa ni vigumu kwa kitu choochote chenye uhai kuishi katika sayari ya GJ 1132b.

Dkt. Southworth anasema, " Tulicho onyesha ni kuwa kuna nyota ambazo zinaweza kuwa na anga na kwa vile dunia au nyota kama hizi ni nyingi, kuna uwezekano kuwa moja kati zao zinaweza kuwa na uhai."

Reactions:

0 comments:

Post a Comment