Monday, 10 April 2017

MWANAMUZIKI AJITOSA BAHARINI KUKWEPA KULIPA BILI YA CHAKULA.


Mwanamume mmoja raia wa Australia ambaye alikuwa na bili kubwa ya kulipa baada ya kupata mlo kwenye mkahawa mmoja aliruka na kuingia baharini ili kukwepa kulipa bili hiyo.

Polisi walimfuata kwa kasi mwanamuziki hiyo ambaya baadaye alisema kuwa alikimbia kumsaidia rafiki yake kujifungua mtoto katika fukwe za bahari.
Alikuwa na bili ya zaidi ya dola 450.
Terry Peck ambaye amefunguliwa mashtaka ya wizi baadaye alidai kuwa chakula hicho hakikua kimepikwa kwa njia inayotakikana.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 33 alifikishwa mahakani leo Jumatatu baada ya kisa hicho kilichotokea katika mgahawa wa Omeros Bros.
Australia si nchi pekee ambapo kuna visa vya wateja kula kwenye mikahawa na kukosa kulipa.
Mwezi uliopita polisi wa Uhispania walimkamata mtu anayeshukiwa kuwa kiongozi wa genge ambalo lilikuwa na tabia ya kula kwenye mikahawa na kisha kutoroka kaskazini mwa nchi.

Kundi hilo liliwajumuisha watu 100 lilikula chakula cha thamnia ya euro 22 katika mkahawa wa Bembibre's El Carmen mwezi Machi na baadaye wote wakakimbia bila kulipa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment