Tuesday, 25 April 2017

VIDEO: MELI YA KIJESHI YA MAREKANI YAWASILI KOREA KUSINI

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda kutokana na majibizano makali na vitisho kati ya Marekani na Korea Kaskazini, ambapo meli ya jeshi la Marekani (USS Michigan) imewasili katika Korea Kusini huku hofu ikiongezeka zaidi kuhusu uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora au silaha za nyuklia.

Meli hiyo yenye uwezo wa kushambulia kwa makombora, imewasili kujiunga na kundi jingine la meli za kivita zinazoelekea eneo hilo ambapo zinaongozwa na meli kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson.
USS Michigan hutumia nguvu za nyuklia na hubeba makombora aina ya 154 Tomahawk na wanajeshi 60 pamoja na meli nyingine ndogo.Aidha, bunge la Seneti nchini Marekani limealikwa kwa kikao cha kupewa habari kuhusu Korea Kaskazini siku ya Jumatano katika ikulu ya White House.
Meli hiyo inatarajiwa kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi pamoja na kundi la meli zinazoongozwa na Carl Vinson, kundi ambalo lilitumwa eneo la Korea kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani.
Hivi karibuni safari ya meli za kivita za Marekani ilizua utata kuhusu iwapo zilikuwa zinaenelekea eneo la Korea, lakini maafisa wa jeshi la wanamaji la Marekani kwa sasa wamesema zinaelekea eneo hilo kama ilivyoamrishwa.
Naye Rais wa Marekani, Donald Trump mapema mwezi huu amesema kwamba atatuma kundi kubwa la meli zenye nguvu.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment