Sunday, 9 April 2017

NAPE AMWOMBA RAIS MAGUFULI KUUNDA TUME…..

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Magufuli  kuunda tume huru ya kuchunguza matukio ya uhalifu, utekaji na uvamizi yanayoendelea hapa nchini.
Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wananchi Jimboni kwake Mtama, amesema kuwa kutokana na matukio ya kihalifu yanavyoongezeka kuna haja kubwa ya kuunda tume hiyo huru ili kuweza kuchunguza na kubaini wahusika.
Amesema kuwa haiwezekani vikundi hivyo vya uhalifu vikawa na nguvu zaidi kushinda vyombo vya dola hapa nchini na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi.
“Ombi langu kwa Rais Dkt. Magufuli namuomba aunde tume huru ichunguze matendo haya yasijirudie tena kwa sababu yasipochukuliwa hatua yataharibu sura ya Tanzania pia yataweza kuibuka makundi ya wahuni kuanza kuteka watu hovyo,”amesema Nape.
Aidha Mbunge huyo amesema watu wanaofanya mambo hayo wanalengo la kuwagombanisha wananchi na Serikali yao jambo ambalo sio zuri kwa taifa.

Hata hivyo, amesema kuwa mpaka sasa haamini yule mtu aliyemtolea silaha siku ya mkutano wake na waandishi wa habari kama alitumwa na hajui vyombo vya Ulinzi na Usalama vinafanya nini mpaka sasa.

Related Posts:

  • MWANAFUNZI AKAMATWA KWA KUMKASHIFU RAIS KWENYE FACEBOOK.... Jeshi la polisi nchini Zambia linamshikilia mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini humo, kwa tuhuma za kumkashifu Rais Edgar Lungu na maafisa wengine wa Serikali kwenye Facebook. Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Esther… Read More
  • BIBI HARUSI AJARIBU KUMUUA MUMEWE BAADA YA NDOA Bibi harusi katika jimbo la Tennessee nchini Marekani, ametiwa nguvuni baada ya polisi kusema kuwa alitoa bunduki kwenye gauni lake la harusi na kumtishia mumewe saa chache tu baada ya kufunga ndoa. Kate Elizabeth Prich… Read More
  • MWIZI AKUTWA AMELEWA NDANI YA NYUMBA ALIOVUNJA…. Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia kwa wizi, baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani. Polisi wanasema jamaa huyo wa miaka 36 alivunja na ku… Read More
  • RAIS MUSEVENI: SIJAUGUWA KWA MIAKA 31 Mara nyingi kumekuwa na ripoti za kuugua kwa marais, hasa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Bwana Buhari amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa ambao haujulikani mjini London tangu mwezi Mei, ambayo ni ziara ya pili anafan… Read More
  • MKUU MPYA WA FBI APATIKANA…… Bunge la Seneti nchini Marekani limepiga kura ya kuthibitishwa Bwana Christopher Wray kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani la FBI. Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu James Comey alipotimuliwa na Rais Dona… Read More

0 comments:

Post a Comment