Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Paul Makonda, ameahidi Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wengine wawili
watapatikana Jumapili hii baada ya wasanii hao kutekwa na watu wasiojulikana
Jumatano hii wakiwa Tongwe Record.
Alisema hayo akiwa
nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam, muda mchache baada ya kutembelewa
na wasanii ambao walimtaka mkuu huyo kuwasaidia kupatikana kwa wasanii hao.
Akiongea na waandishi
mbele ya wasanii hao, RC Makonda alisema kila mtanzania ana nafasi ya kumtafuta
Roma na wenzake kwa kuwa hakuna anayejua watu hao wako wapi.
0 comments:
Post a Comment