Saturday, 1 April 2017

RAIS MAGUFULI AIPASUA KICHWA TANESCO……

Ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia hapa nchini imetoa changamoto kubwa kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kuliagiza Shirika hilo kuweka mikakati madhubuti ya kuzalisha na kuuza umeme kwa bei nafuu.

Rais Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo Jijini Dar es salaam wakati wa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn ambaye yuko hapa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, amesema kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia ameahidi kuipatia Tanzania umeme megawati 400 kwa ajili ya kusambaza nchini.
Aidha, Desalegn amesema kuwa atatoa ofa ya megawati 400 kwa ajiri ya kusambaza nchi nzima, kwani Ethiopia umeme unauzwa kwa bei ndogo ya senti sita, hali ambayo ilipelekea kwaRais Magufuli kuliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kujifunza kile ambacho Ethiopia inafanya ili waweze kuzalisha umeme wa bei nafuu.
“Hii itakuwa ni hatua nyingine ya Tanesco kujifunza namna Ethiopia wanavyozalisha umeme na kuuza kwa bei nafuu na wao waanze kufanya hivyo,”amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia ameahidi kufungua ubalozi hapa nchini na kuahidi kumpa eneo Mjini Dodoma.

Related Posts:

  • MLANGO WA BOMBARDIER WAZUA TAHARUKI ANGANI…! Abiria waliokuwa wakisafiri kwa ndege aina ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Mwanza kuelekea Dar es salaam, walipata hofu baada ya ndege yao kuruka na muda mfupi baadae kulazimika kutua tena ka… Read More
  • MAJAJI WAJINOA MAHAKAMA YA UFISADI…!! Jaji Mkuu wa tanzania Mohamed Chande amesema kuwa, jopo la majaji linatarajiwa kuingia darasani ili kujifunza sheria mpya ya kuendesha kesi za ufisadi.  Kesi hizo zitakuwa zinaendeshwa katika Mahakama Kuu Kite… Read More
  • MJI WA MADINA WASHAMBULIWA…!! Mshambuliaji mmoja wa kujitoa mhanga, amejilipua katikati ya Jiji la Media jirani na Msikiti wa Mtume. Jiji la Medina ni miongoni mwa miji mitakatifu, kwa mujibu wa Imani za dini ya Kiislamu. Kituo cha Televisheni… Read More
  • FARU MPYA AWEKA REKODI NGORONGORO..!! Mnyamapori aina ya faru anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko faru wote duniani, anaishi katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha. Faru Fausta mwenye umri wa miaka 54, ni miongoni mwa faru weusi ambao asili yao ni … Read More
  • MEXICO: HATUTALIPIA UKUTA WA DONALD TRUMP..!! Nchi ya Mexico imesema kuwa haitalipia gharama ukuta uliopendekezwa kujengwa, na rais wa Marekani Donald Trump. Kauli hiyo imetolewa na rais wa taifa hilo Enrique Pena Nieto kupitia Runinga nchini humo,huku akishutumu… Read More

0 comments:

Post a Comment