Wahudumua wa ndege ya shirika la ndege la Uturuki,
walisherehekea kuwasili kwa abiria mwingine angani umbali ya futi 42,000 au
mita 12,800, wakati mwanamke mmoja alijifungua mtoto msichana.
Abiria nao walisaidia
kuzaliwa kwa mtoto huyo, muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji mkuu
wa Guinea, Conakry, ikielekea Isanbul kupitia Burkina Faso.
Mama wa mtoto huyo
aliyepewa jina Kadiju, walipelekwa hospitali wakati ndege hiyo aina ya Boeng
737 ilipotua mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.
Wote waliripotiwa
kuchoka lakini walikuwa na afya nzuri.
![]() |
Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege angani |
Wahudumu waligundua
kuwa mwanamke mmoja abiria kwa jina Nafi Diaby, alikuwa akihisi uchungu wa
kujifungua.
Hapo ndipo walichukua
hatua ya kumsaidia kujifungua ndege ikiwa safarini.
Mashirika mengi ya
ndege huruhusu mama walio wajawazito wa hadi wiki 36 kusafiri, lakini uhitaji
barua ya daktari wakifikisha wiki 28 kuonyesha tarehe wanayotarajia kujifungua.
0 comments:
Post a Comment