Sunday 9 April 2017

MLIPUKO WAWAUA WATU 13 KANISANI MISRI..

Takriban watu13 wameuwa kwenye mlipuko uliotokea katika kanisa moja kaskazni mwa Misri.

Mlipuko huo ulilenga kanisa la St George's Coptic, lililo mji wa Tanta huko Nile Delta.
Vituo kadha vya runinga vilisema kuwa takriban watu 40 walijeruhiwa.
Chanzo ya mlipuko huo bado hakijulikani lakini jamii ya wakiristo wachache nchini Misri wamekuwa wikilengwa na wanamgambo wenye itikadi kali.
Mwezi Disemba mwaka uliopita, watu 25 waliuawa wakati bomu lilipolipuka katika kanisa la Coptic cathedral mjini Cairo wakati wa sala.
Ghasia dhidi ya wakiristo wa Coptic, zimekuwa nyingi miaka ya hivi karibuni, hasa tangu mwaka 2013 wakati jeshi lilipompindua rais aliyekuwa amechaguliwa.

Baadhi ya wafuasi wa rais aliyetimuliwa Mohammed Morsi, ambaye alitoka kundi la Muslim Brotherhood, waliwalaumu wakiristo kwa kuunga mkono kupinduliwa kwake.

0 comments:

Post a Comment