Sunday 9 April 2017

MBARONI KWA KWA UBAKAJI…

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Samweli Masumbuko (32), Mkazi wa Kata ya Mahina wilayani Nyamagana, kwa tuhuma za kumbaka  mwanafunzi wa darasa la pili (jina linahifadhiwa) mwenye
umri wa miaka 10.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 1, mwaka huu saa 11:00 jioni katika Mtaa wa Mwembeni,Kata ya Mahina.
Kamanda Msangi alisema mtuhumiwa anadaiwa kuwa alimbaka mwanafunzi huyo Machi 25, mwaka huu saa 11:00 jioni, lakini kwa kipindi chote hicho hakuweza kusema kwa mtu yeyote hadi Aprili 1, mwaka huu mama  yake alipogundua mwanawe kufanyiwa ukatili huo.

Alisema upelelezi dhidi ya watu waliohusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha au kushawishi ukatili huo bado unaendelea na kwamba mtuhumiwa anahojiwa na Jeshi la Polisi na pindi uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

0 comments:

Post a Comment